Monday, January 30, 2012
BWANA ANAKUPIGANIA
Ndugu yangu,
Tumsifu Yesu Kristo,
Habari ya siku hii nzuri ya Leo? Leo nataka nichukue nafasi hii kusema nawe jambo moja kwa ufupi lakini ni Kubwa sana ambalo nimejifunza asubuhi ya leo.
Neno hili latoka katika Yeremia 50:25 / Jeremiah 50:25
"The LORD hath opened his armoury, and hath brought forth the weapons of his indignation: for this [is] the work of the Lord GOD of hosts in the land of the Chaldeans"
"Bwana amefungua akiba yake ya silaha, naye amezitoa silaha za ghadhabu yake; maana Bwana,
Bwana wa majeshi, ana kazi atakayofanya katika nchi ya Wakaldayo."
Hayo ndiyo asemayo Bwana, NI kwamba mara nyingi na hususani Wakristo twaamini kuwa Mungu hutupigania maeneo tofauti tofauti, kwa Nyakati tofauti tofauti, na namna tofauti. hili ni jambo jema sana
Ndugu yangu Mungu wetu ni Mkuu na anao uwezo juu ya kila kitu unchoweza fikiria katika Ulimwengu huu, na pia ana uwezo wa kukupigania vita ya aina yoyote ile unayoweza ifikiria, na hata ile usiyoijua (maana viko vita vingi sana ambavyo Mungu hutupigania pasipo sis wenyewe kujua)Na silaha zetu tulizopewa zina nguvu kwenye falme, mamlaka na kupigana na roho wabaya etc (effeso 6:11)
Kitu cha pekee na Tofauti katika Neno la Leo ni kuwa Mungu pamoja na uweza wake wooote tunaoweza fikiria Bado anafungua ghala zake, akiba zake za silaha ili afanye Kitu kwa ajili yako na mimi akapigane na watesi wetu. pata picha ya jeshi ambalo umezoea kuwaona na silha za kawaida lakini zikakutisha vipi wakichukua na zilizo kwenye akiba???
Hebu angalia hapa pia Yeremia 50:34 "Mkombozi wao ni hodari; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli" Hapo ni muendelezo wa alichosema katika Mstari 25. Kwa msomaji wa Biblia aweza kuwa anajua kuwa Mungu anapojitambulisha "BWANA WA MAJESHI" anamaanisha hapo kuna vita ya kukupigania.
Pamoja na kufungua hadi silaha za akiba ili kupigana na adui/watesi wako, yeye Mwenyewe ndiye Mkombozi wako, na ATAKUTETEA KWA BIDII, aistareheshe Nchi!!
Ndugu yangu Mungu akubariki sana, ninakuombea Mungu akusaidie kuona zaidi ya kile nilichoanza kwa kutafakari hapa pamoja nawe katika Neno hili.
Na kama una vita ambayo unaipitia jipe Moyo maana aliye pamoja nasi Ni MKUU sana, na anaaweza yooooote!!
Ubarikiwe, kwa maoni/ maombi ingia hapo chini kwenye kibox kilichoandikwa maoni, sio lazima unadike jina lako. ubarikiwe sana
Mungu akubariki hii wiki yote, akutangulie, akusaidie, na akuinue pia.

Monday, January 23, 2012
Kumtumikia Mungu: Fanya kwa moyo na utabarikiwa, fanya kwa ulegevu na Utalaaniwa
Wapendwa wangu Tumsifu Yesu Kristo,
habari ya leo?
katika mfululizo wa Neno la siku, leo nimeguswa sana na Neno kuhusu kumtumikia Mungu
Najua wapo watu wengi wana kiu mbali mbali za kumumikia Mungu kwa namna mbalimbali, na ninajua wanaweza kuwa wapo pia wale ambao hawajui wataanzaje kumtumia mungu
1. Nini tunamaanisha tunaposema Kumtumikia Mungu
tunajua kuwa miito ipo mingi na kwa namna mbalimbali sana! na ndiyo maaana tunapoongelea habari ya kumtumikia Mungu, napenda wazo la kwanza kuingia akilini mwako liwe ni namna unavyomtukuza Kristo katika mazingira yanayokuzunguka, ama jinsi unavyomuinua Kristo katika hiyo kazi yako ama majukumu ya Kristo. japo pia zaidi tutaongelea pia habari ya kufanya kazi juu ya Ufalme wa Mbinguni, ili katika lile unafanya liweze kuwa sifa na utukufu kwa Mungu wetu wa Mbinguni.
2.Matokeo (reward za kumtumikia Mungu)
"26Mtu ye yote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba Yangu atamheshimu" Yohana 12:26
Kwanza Kabisa mtu kama anataka kumtumikia Kristo, lazima ajikane mwenyewe na kumfuata Kristo. kumbuka Kumtumikia Mungu sio option, bali ni jukumu lako la kawaida kabisa kama Mkristo unayemuamini na kumfuata Kristo. si jukumu la watu fulani tu ama watu wa hadhi fulani tu.
Kuna baadhi ya watu wao hujiona kuwa "eti" ni "wachanga" Naomba ujue kuwa katika hali hiyo uliyonayo hata kama umemuamini Yesu Kristo leo asubuhi bado Una nafasi ya Kumshuhudia Kristo na kuutukuza ufalme wake na kwa wanadamu wengine pia.
Kizuri ni kuwa Mungu wetu si dhalimu kama asemavyo katika Waebrania 6:10-12 "10Mungu si dhalimu, hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili Yake katika kuwahudumia watakatifu na kama vile mnavyoendelea kuwahudumia. 11Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, 12ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi." Kwa tafsiri nyingine inasema Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu.... Ninachomaanisha kama alivyosema katika Yohana kuwa Mungu atamuheshimu yeye amtumikiaye!! Yaani Mungu, Mumba mbingu na nchi anakuheshimu wewe!! waoh what a good news here!!
na hakuishia hapo tu ila akaendelea na kusema katika Isaya 52:13 "13Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima, atatukuzwa na kuinuliwa juu na kukwezwa sana"
Hii inamaanisha kuwa Kumtumikia Mungu kunafanya wewe uwe Unnormal (though not ubnormal) Kwanza Mungu anakuheshimu, pili Unainuliwa juu sana, na bado Utukufu wako upo
Hakika naomba tufanya kile ambacho MUngu anatutuma kufanya, wengine tunatamani kumtumikia kwa pesa zetu, kwa maana tupo tayari kufanya hivyo ili Injili iende, wengine kwa kutoa muda wetu, wengine kwa maombi na kila mtu kwa namna mbali mbali, ndugu yangu usiwe mvivu ili usije ukaikosa hii opportunity!!
Pamoja na neema hizo hapo juu lakini PIa Mungu anaonya kwa wenye kumtumikia kwa ulegevu "Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu..." Yeremia 48:10
Ndugu yangu, wapo watu wengi kwa kusahau kuwa kazi ya Kumtumikia Mungu ina vita na upinzani mwingi wamejikuta wakirudi nyuma ama wakitumainia akilia zao, ama wakipunguza kasi waliyoanza nayo hapo mwanzoni, asilimia kubwa ni kutokana na kutaka kujichukulia umaarufu, kujitukuza wao, Tamaa za mwili (uzinzi, njaa, uvivu etc, pesa, kubanwa na shughuli nyingi "busy" na sababu nyingie mbalimbali, na hata baadhi kutokuwa tayari kuachilia baadhi ya vitu ama vitabia kwenye maisha yao.
Ndugu kama hujataka kujikana mwenyewe halafu unajiita wewe ni mtumishi hatari ya laana inakusubiri hapo mbele yako, bora uchague moja, Mtumikie Mungu kwa moyo wako woooote naye atakulipa kwa namna anayoijua Yeye kwa wakati wake na utshangaa.
Ubarikiwe sana Ndugu yangu, kama unajisikia kuongeza kitu katika mada hii karibu hapo chini kwenye maoni acha maoni yako hapo.
Nakuombea Mungu akubariki katika utumishi aliokuitia, mtumikie Bwana pasipo kuchoka ndugu yangu, utaurahia upendo wake na Fadhili zake nyingi tu!
Sunday, January 15, 2012
Bye Regia. Pole Mzee Mtema
Ni msiba wa ghafla sana ambao umetufikia. Binafsi, namuona Regia kama Mbunge kijana, model kwa vijana wenzake wengi, mmoja wa walemavu waliothubutu kuonyesha kuwa wanaweza na pia ni muinjilishaji na mtoto wa Mzee wetu Mzee estelatus Mtema ambaye ni mratibu wa shughuli za Catholic Charismatic renewal Tanzania.
napenda nitoe pole kwa woooote tulioguswa na msiba huo, kwanza kwa wananchi wa kilombero, pili kwa wakarismatiki wenzake wooote, na tatu kwa MZee wetu Mtema. poleni sana
ni kweli kuna misiba mingi ya watu maarufu inatukuta, lakini huu umenigusa sana.
ninakumbuka mwaka jana siku moja nilikuwa nachat naye kwenye Facebook na hiki ndicho aliniambia kama inavyoonekana!!
Good bye Regia, Pole mzee Mtema.
Friday, January 6, 2012
Catholic charismatic renewal - Spiritual retreat 2011/2012
The Catholic Charismatic renewal in the Arch-diocese of Mwanza, held a three day retreat for the Youths and college students from SAUT Mwanza. This wonderful event involved Leadership studies, Prayers, evaluation of 2011 and planning for 2012.
The event took place at St. Martin Formation and training center in Kahangara Magu Mwanza.
down here are some pics for the event
Karismatiki Katoliki Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, iliandaa mafungo ya siku tatu kwa vijana na wanafunzi kutoka chuo kikuu cha SAUT Mwanza. Tukio hili zuri lilihusisha masomo ya uongozi, Maombi, Tathmini ya mwaka 2011 na kuweka mipango kwa ajili ya 2012
Tukio hili lilifanyika katika kituo cha Mafungo cha ST. Martin Kahangara Magu Mwanza
Chini happo ni baadhi ya picha za baadhi ya washiriki na wakufunzi waliofundisha katika mafungo hayo
Hapa ni siku walipofika Kahangara, baadhi ya wanakamati ya Huduma ya vijana na vyuo kwa Jimbo la mwanza mara baada ya kufika eneo la tukio na kuanza kwa kumsifu Mungu
Hapa Kaka Albert akijiandaa kuendelea na kipindi cha Maombi
baadhi ya washiriki wakifuatilia kipindi cha usiku baada ya Dinner
Kaka Deus akiendelea na kufundisha juu ya uongozi
Mwenzetu dada Regina yeye siku ya kumaliza mafungo, tarehe 1/1/12 hakuwa akijisikia vizuri hivyo akawa amepumzika hostel kwake, hivyo baada ya kutoka kanisani tulienda kumsalimia tukiongoza na Mratibu wa Karismatiki Katoliki JImbo kuu Katoliki La Mwanza, Kaka Stani. PIchani Juu ni Dada Regina akiwa amekumbatiwa na mumewe Kaka Jenes Kanje
Moja kati ya waheni wakubwa waliofika katika Mafungo hayo ni pamoja na Mratibu wa Karismatiki Katoliki Jimbo kuu la Mwanza, Kaka Stani Matani. alifika na kufundisha jinsi ya vijana kutumia opportunities zilizoko kwa ajili ya kupeleka INjili. Pamoja na Kaka Stani, pia Tulitembelewa na Fr. Madatta ambaye ni Mlezi wa vijana Karismatiki Mwanza, pia Fr Andrea, ambaye ni paroko wa Kahangara.
Surely ilikuwa ni event nzuri sana.... tarehe 1/1/12 jioni saa 12 ndipo iliisha but ilikuwa kama watu wana hamu waendelee tu...... ilihusisha jumla ya watu 18 kutoka SAUT, Mwanza mjini na Tarime

Subscribe to:
Posts (Atom)